Mwanaume aliyemuua Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe, amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Tetsuya Yamagami alimpiga risasi Abe wakati wa mkutano wa kampeni mjini Nara miaka mitatu na nusu iliyopita. Ingawa alikiri kosa lake, adhabu hiyo imezua mjadala nchini Japan, ambapo baadhi wanamwona kama muuaji katili huku wengine wakimhurumia kutokana na maisha yake ya nyuma.
Mauaji hayo yaliishtua Japan, nchi yenye viwango vya chini sana vya uhalifu wa bunduki.