Kijana kutoka Brazil anazidi kung'ara kwenye klabu ya Olympique Lyonnais Endrick inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa hii ni mara baada ya leo January 25,2026 kupiga mabao matatu kwenye ushindi wa 5-2 ambao Lyonnais wameupata dhidi ya Metz.

Endrick ambaye yupo klabuni hapo kwa mkopo akitokea klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania amekuwa na wakati mzuri sana ndani ya Lyno toka kutambulishwa kwake ambapo alishinda kwenye mchezo wake wa kwanza.

Mpaka sasa Endrik anaidadi ya mabao manne (4) ambayo ameifungia klabu hiyo toka ajiunge nayo. Endrik hakuwa na wakati mzuri ndani ya Madrid jambo ambalo lilimfanya atolewe kwa mkopo na miamba hao wa Hispania.