Manchester United yamchapa Arsenal nyumbani kwake (2-3)

-rickmedia: Rick

Rick

14 hours ago
rickmedia: manchester-united-yamchapa-arsenal-nyumbani-kwake-2-3-868-rickmedia

Ni wikiendi ya maumivu makali kwa mashabiki wa Arsenal hii ni mara baada ya Manchester United kuvuruga furaha yao ndani ya Uwanja wao wa Nyumbani (Emirate) kwa kukubali kuchapwa mabao 3-2 na Man United.

Arsenal walianza kwa kupata furaha baada ya Man United kujifunga kufuatia shambulizi lililoanzishwa na Saka kisha mpira kumgonga Martinez na kuingia kambani.

Man United hawakukata tamaa, walipambana kupitia Mbeumo walisawazisha Goli. Dakika ya 50" Dorgu anawaamsha tena mashabiki wa Man kwa kupachika bao la roho mbaya. Dakika ya 84" Mikel akawarudisha tena Arsenal kwenye mchezo na kufanya mchezo kuwa 2-2.

Dakika 3" kabla ya kumalizika kwa dakika 90" za mchezo Cunha akazima ndoto za Arsenal kwa kupachika bao la 3 kwa Man United. Full Time Arsenal 2-3 Manchester United.

Matokeo haya yanawapandisha Man United nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza huku Arsenal akibaki kileleni na alama zake 50 nyuma akiwa Man City ambaye amepungukiwa alama 4 tu kumfikia Arsenal.