Rwanda watuma maombi ya kuandaa mashindao ya mbio za magari 'F1'

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 week ago
rickmedia: rwanda-watuma-maombi-kuandaa-mashindao-mbio-magari-f1-545-rickmedia

Rais wa Rwanda 'Paul Kagame' alitangaza kuwa Rwanda imewasilisha ombi la kuandaa mashindano ya mbio za magari 'Formula 1' na mazungumzo kuhusu jambo hilo yanaendelea vizuri.

Alitangaza habari njema hiyo leo hii wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la FIA.

Agosti mwaka huu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Formula One Stefano Domenicali alisema kuwa mkutano huo utafanyika nchini Rwanda kuangalia mpango wa nchi hiyo kuwa mwenyeji wa mbio hizo za magari yenye kasi na ghali zaidi duniani.

Kama ombi hili litapitishwa Rwanda itakuwa nchi ya kwanza Afrika mashariki kuandaa mashindano haya ambayo ndio mashindano makubwa zaidi ya mbio za magari Duniani.