Rapa na mfanyabiashara Jay Z "HOV" amesalia kuwa msanii pekee wa HipHop ambaye ameorodheshwa katika list ya watu maarufu waliofikia hadhi ya Ubilionea katika jarida la Forbes.
Inatajwa kuwa utajiri wa JayZ unakadiriwa kuwa wa Dola Bilioni 2.5 sawa na Tsh Trilioni 6,375,000,000,000. hii ni kupitia biashara zake mbalimbali anazomiliki ikiwa ni pamoja na zile za ndani ya kiwanda cha muziki pamoja na nje ya kiwanda cha muziki.
Ikumbukwe utajiri huu ni wa Jay Z peke yake bila kujumlisha na ule wa mke wake 'Beyonce' ambaye wiki kadhaa zilizopita yeye pia alitajwa kama ni Bilionea rasmi.
Wakati unatafuta mtu wa kuingia naye kwenye ndoa hakikisha wote mna ari ya utafutaji inayofanana ili mpate mafanikio na kufurahia kwa pamoja.