Rais Samia aomboleza kifo cha Mwasisi wa CHADEMA James Matei

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: rais-samia-aomboleza-kifo-cha-mwasisi-chadema-james-matei-998-rickmedia

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi baada ya kifo cha mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei (94).

Mtei aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Januari 20, 2026 jijini Arusha, akiwa na umri wa miaka 94.

Rais Samia ametuma salamu hizo, leo Jumanne Januari 20, 2026 kupitia taarifa iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu pamoja na kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Samia amepokea kwa masikitiko, taarifa za kifo cha Mzee Edwin Mtei.