Juma Lokole akerwa na tabia ya Wema Sepetu kukimbia kazi sababu ya Whozu

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: juma-lokole-akerwa-tabia-wema-sepetu-kukimbia-kazi-sababu-whozu-503-rickmedia

Mtangazaji na Mwanamitandao ya Kijamii Juma Lokole amemtolea uvivu Miss Tanzania Mwaka 2006 Wema Sepetu ambaye pia ni rafiki yake, Lokole ameweka wazi kuwa alimpatia kazi Wema ya kwenda naye pamoja nchini Kenya ambapo walitakiwa kurudi leo hii January 21, 2026 lakini baada ya kurudiana na Whozu hakuonekana eneo la kazi.

Kwenye mahojiano (Interview) aliyofanya na Saraphina Jerry, Juma Lokole ameongea kwa hisia kali akisema Wema amemkosea sana na anajutia kumpa kazi hiyo bora angempa Kajala kazi hiyo huku akisisitiza kuwa mastaa wa Tanzania watabaki kuyaona mafanikio ya Hamisa Mobetto na Nana Dollz sababu wanaziheshimu kazi na hawaachi kazi.

Itazame Hapa Chini Interview Ya Juma Lokole👇