Bad Bunny avunja rekodi ya Super Bowl kwa kupata likes nyingi

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

16 hours ago
rickmedia: bad-bunny-avunja-rekodi-super-bowl-kwa-kupata-likes-nyingi-762-rickmedia

Bad Bunny ameandika historia mpya kwenye Super Bowl Halftime Show 2026 baada ya teaser yake kuvunja rekodi ya mitandao ya kijamii. Ndani ya saa chache tu baada ya kutolewa, video hiyo ilifikisha likes milioni 3, ikivuka rekodi ya mwanzo ya Rihanna ya likes milioni 2.9.

Kufikia siku ya tatu, teaser hiyo tayari imekusanya likes milioni 4, ikiendelea kuongoza kama video ya Super Bowl Halftime Show yenye mapokezi makubwa zaidi kuwahi kutokea.

Rekodi hii inaonyesha nguvu kubwa ya mashabiki wa Bad Bunny na mvuto wake wa kimataifa kabla ya shoo yake kubwa Februari 8, 2026.