Samuel Eto’o alielewa kitu ambacho wengi hawakielewi kusaidia sio lazima kumaanishe kutoa pesa. Badala ya kuwapa ndugu au marafiki wa karibu hela, Eto’o huuliza swali moja muhimu; “Unataka kufanya nini na maisha yako?”
Ukisema biashara, hakupi pesa ya matumizi. Anakusaidia kuanzisha biashara yenyewe.
Eto’o anaamini misaada ya muda mfupi huisha haraka, lakini ujuzi, umiliki na fursa hudumu kwa vizazi. Kumpa mtu pesa kunaweza kumsaidia leo, lakini kumpa njia kunambadilisha maisha yake ya baadaye.
Huo ndio uongozi wenye maono.
Hivyo ndivyo urithi wa kweli hujengwa.