Simba imemtangaza mlinzi wa kati, Ismael Toure kama mchezaji wake mpya akiwa mchezaji huru.
Toure mwenye umri wa miaka 28, anmudu kucheza nafasi za beki wa kati na pia kiungo mkabaji.
Mchezaji huyo raia wa Ivory Coast anasajiliwa kuziba nafasi ya Chamou Karaboue ambaye klabu hiyo itaachana naye katika dirisha hili dogo la usajili.