Rais wa zamani wa Burkna faso 'Paul-Henri Sandaogo Damiba' arudishwa nchini kwao

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: rais-zamani-burkna-faso-paul-henri-sandaogo-damiba-arudishwa-nchini-kwao-681-rickmedia

Serikali ya Togo imemrudisha nyumbani Paul-Henri Sandaogo Damiba, rais wa zamani wa Burkina Faso, kufuatia ombi la mamlaka ya nchi hiyo.

Damiba, aliyekuwa akiishi uhamishoni Togo tangu kupinduliwa kwake mwaka 2022, anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za umma.

Alikamatwa tarehe 16 Januari 2026 akihusishwa na jaribio la kumpindua kiongozi wa sasa, Kapteni Ibrahim Traoré.