Rais wa Guatemala, Bernardo Arévalo, atangaza hali ya hatari nchini kwake

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

16 hours ago
rickmedia: rais-guatemala-bernardo-arevalo-atangaza-hali-hatari-nchini-kwake-773-rickmedia

Rais wa Guatemala, Bernardo Arévalo, ametangaza hali ya hatari ya siku 30 kote nchini kufuatia mauaji ya maafisa wanane wa polisi yanayodaiwa kufanywa na magenge ya kihalifu.

Akihutubia taifa, amesema vyombo vya usalama tayari vimerejesha udhibiti wa magereza matatu yaliyokuwa yametekwa na magenge hayo mwishoni mwa wiki. Serikali inalenga kurejesha usalama na kudhibiti uhalifu nchini.