Kwa mara ya kwanza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshusha Mabasi 10 ya abiria ambayo yatakuwa yanatumia umeme kwenye uendeshaji wake.
Ujio wa Mabasi hayo ni muendelezo wa kuhakikisha uboreshwaji wa sekta ya usafiri Visiwani humo. Ujio wa Mabasi haya utakwenda kupunguza gharama za uendeshaji lakini pia urahisi wa usafari kwenye Visiwa hivyo vinavyopokea mamilioni ya Watalii kila mwaka.
Awamu ya kwanza ya mradi wa Mabasi yanayotumia Umeme (Zan Bus) imewasili kupitia Bandari ya Malindi, Zanzibar, na kuelekea katika maegesho ya Stendi Mpya ya Kijangwani, Mkoa wa Mjini Magharibi.