Msanii wa hip hop na muigizaji 50 Cent amesema hachanganyi masuala ya siasa na dini katika kazi zake za filamu kwa kuhofia kuharibu mwelekeo wa kazi yake.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa filamu “Moses The Black”, 50 Cent alisema kugusa maeneo hayo kunaweza kuleta madhara, akiwataja Kanye West na Nicki Minaj kama mifano ya wasanii waliokumbana na changamoto baada ya kujihusisha na masuala hayo.
Kiukweli ukiachana na kauli hiyo ya 50 Cent ukweli uko wazi kuwa Kanye West kujiingiza kwenye masuala ya dini kwa ukubwa ilimpa matatizo na baadhi ya mashabiki zake huku kwa upande mwingine Nicki Minaj bado analihisi joto la jiwe baada ya kujiingiza kwenye siasa mpaka sasa baadhi ya watu wanataka arudishwe kwao huko Trindad.
Kwahiyo haya yote yamempa funzo kubwa sana 50 Cent ambaye hataki kabisa kuhusisha vitu hivyo kwenye kazi zake.