A$AP Rocky ameweka wazi maelezo kuhusu uhusiano wake na rapa Drake, akithibitisha kuwa hawako sawa lakini beef yao inahusiana na historia ya mapenzi na wanawake, sio vita vya moja maana sana.
Akizungumza kwenye mahojiano na Oldman Ebro, A$AP Rocky alisema kuwa tofauti hizo ziliibuka baada ya marafiki kuwa wapinzani kutokana na hisia binafsi na historia ya mapenzi. Alisisitiza kuwa wimbo wake mpya, “Stole Ya Flow”, sio diss rasmi kwa Drake, bali ni kwa yeyote anayejiona kuguswa.
Mashairi ya wimbo huo yanayomgusa Rihanna yamechochea mjadala mtandaoni, kutokana na historia ya kihisia kati ya Rihanna na Drake, na sasa Rihanna ni mpenzi na mama wa watoto wa A$AP Rocky. Hata hivyo, A$AP Rocky amebainisha kuwa Rihanna sio chanzo cha bifu yao moja kwa moja.