Ratiba yako ya mwaka huu 2026 ikoje mpaka sasa?,imejaa? au bado hujapanga kabisa? Sasa kama wewe bado jua Msanii #Davido ameweka ratiba yake wazi kuwa yupo busy na show mpaka mwezi wa tano kwasasa na bado kuna uwezekano wa kuwa busy mwaka mzima.
Uongozi wa msanii huyo umepost ratiba ya shows za msanii huyo ambazo zinaanza mwezi wa pili mpaka mwezi wa tano kwa nchi tofauti ndani ya Afrika na nje ya Afrika.
Katika ratiba hiyo ya Davido pia kuna show anayotarajia kuifanya nchini Tanzania February 7, 2026 pamoja na show yake ya nchini Zambia anayotarajia kuifanya May 2,2026.

Hii ni muendelezo wa Ziara (Tour) yake aliyoipa jina la #5IVEAliveTour!! 5️⃣