Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza kuifungua tena njia ya Gaza Rafah kwaajili ya abiria tu ambao watatumia njia hiyo kuelekea Misri.

Hatua hiyo imetangazwa baada ya Israel kukamilisha utafutaji wa mateka waliotekwa na kikundi cha HAMAS. Mpaka huu ulipaswa kufunguliwa mapema baada ya mazungumzo ya kwanza na Rais wa Marekani Donald Trump ambaye alidhamiria kuimaliza mapigao hayo.
Mateka wote waliotekwa na HAMAS walirudishwa kasoro mwili wa Polisi mmoja aliyetambulika kwa jina la Ran Gvili. Majeshi ya Israel yalitangaza kuwa yalifanya mashambulizi Kaskazini mwa Gaza katika kuhakikisha wanaupata mwili wa Polisi huyo.