Harmonize aandika Historia nchini Ethiopia, Apiga Bonge la Show

-rickmedia: Rick

Rick

7 hours ago
rickmedia: harmonize-aandika-historia-nchini-ethiopia-apiga-bonge-show-263-rickmedia

Usiku wa jana mwanamuziki Harmonize amefanya show nchini Ethiopia kwenye moja ya Tamasha kubwa sana nchini humo linaloshirikisha wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Ethiopia.

Kwenye show hiyo Harmonize amepata shangwe la kutosha huku nyimbo zake za "KAINAMA" na "SINGLE AGAIN" zikiwa ndio nyimbo pendwa zaidi kwa mashabiki waliojitokeza usiku huo.

Show hiyo imefungua milango kwa Harmonize na kuamua kuandaa ziara maalumu ya kuzunguka nchi mbalimbali Barani Afrika ambapo itasindikizwa na Album yake mpya "31" anayotarajia kuitoa mwaka huu 2026