Justin Bieber, amem-unfollow rafiki yake wa muda mrefu na mshauri wake, Usher, kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Hatua inayoibua mjadala mkubwa kwa mashabiki, hasa ikizingatiwa uhusiano wa karibu wa muda mrefu kati ya wawili hao.
Hii sio mara ya kwanza kwa Bieber kuchukua hatua kama hizi, kwani pia ameripotiwa kuwa amewa-unfollow watu wengine muhimu kwenye maisha yake ya muziki, akiwemo meneja wake wa muda mrefu, Scooter Braun, ambaye pia amefuta akaunti yake ya Instagram.
Sio Usher wala Bieber hawajatoa tamko rasmi kuhusu suala hili, lakini mashabiki wanahisi huenda kuna mabadiliko makubwa kwenye maisha binafsi na kazi yake Justin Bieber.