Bondia Hassan Mgaya afariki Dunia baada ya kupigwa TKO

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 days ago
rickmedia: bondia-hassan-mgaya-afariki-dunia-baada-kupigwa-tko-524-rickmedia

Bondia Hassan Mgaya amefariki siku moja baada ya kupigwa TKO katika pambano la raundi 6 lililofanyika Tandale kwa Mtogole katika ukumbi wa Dunia Ndogo, ambapo alipoteza fahamu dakika chache baadaye

Imeelezwa kuwa alipelekwa Hospitali ya Sinza kwajili ya matibabu na kutokana na hali yake kubadilika, alipewa rufaa ya kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambako umauti ulimkuta.

Mgaya alicheza pambano hilo ambalo halikuwa la ubingwa, Desemba 28, 2024 lililomkutanisha na mpinzani wake, Paulo Elias.