Harmonize Afunguka Kuhusu Kurudiana na Kajala

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

5 days ago
rickmedia: harmonize-afunguka-kuhusu-kurudiana-kajala-799-rickmedia

Baada ya Kuwepo kwa Stori kuwa Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Rajab Abdul Kahali Maarufu kama #HARMONIZE na Alekuwa mpenzi wake Muigizaji Kajala Masanja wamerudiana kisirisiri, Harmonize ameibuka na kufunguka kuhusu maneno hayo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram (Insta Story) Harmonize amewahoji wanaozungumza hayo maneno kama wana uhakika na wanachokisema.

Kwa sasa Msanii Harmonize yupo Single baada ya kuachana na Mpenzi wake anaefahamika kwa jina la Poshy Queen na hii imethibitishwa na pande zote mbili.

Kajala na Harmonize waliachana miezi michache baada ya kuvalisha na Pete kisha badae walirudiana na kuendeleza mahusiano yao mpaka walipogombana tena na kuachana Mwaka 2023.