Kesi ya Kanisa kumnyang'anya zawadi mtoto wa Askofu Sepeku kusikilizwan leo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: kesi-kanisa-kumnyanganya-zawadi-mtoto-askofu-sepeku-kusikilizwan-leo-108-rickmedia

Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi leo Juni 26, 2025 itaendelea na usikilizwaji wa kesi ya ardhi iliyofunguliwa na mtoto wa Askofu John Sepeku, Bernardo Sepeku (63).

Bernado alifungua kesi dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Jackson Sosthenes na mwekezaji huyo, Xinrong Plastic Waste Industry Co Ltd.

Katika kesi hiyo ya ardhi namba 378/2023, Bernado ambaye ni msimamizi wa mirathi ya baba yao anapinga kunyang’anywa zawadi ya kiwanja alichopewa baba yao. 

Anaiomba Mahakama iamuru alipwe Sh3.72 bilioni ambayo ni fidia ya hasara ya kifedha iliyopatikana kutokana na uvamizi wa mali ya ardhi katika kiwanja hicho.

Pia, anaiomba alipwe Sh493.65 milioni kama fidia ya hasara ya mazao yaliyoharibiwa katika shamba hilo.