"Senegal wana haki ya kukata rufaa" Motsepe

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: senegal-wana-haki-kukata-rufaa-motsepe-561-rickmedia

 Sakata la Senegal kunyang'anywa Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (AFCON) na Morocco kupewa ushindi wa mezani wa mabao 3-0, suala ambalo limeibua mjadala kila kona hasa kwa wadau wa soka, mapya yameibuka ambapo Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesema Senegal wana haki ya kukata rufaa na CAF itaheshimu uamuzi wowote utakaotolewa na chombo cha juu zaidi.

Motsepe ameeleza haya kufuatia wito wa Serikali ya Senegal kutaka uchunguzi wa kimataifa juu ya tuhuma za rushwa michezoni, huku akibainisha kwamba kulikuwa na maamuzi tofauti kati ya Bodi ya Nidhamu na Bodi ya Rufaa na Wajumbe hao wa Bodi wanachaguliwa kutokana na mapendekezo ya nchi wanachama 54 wa CAF, na wanajumuisha wataalamu wenye heshima kubwa wakiwemo Majaji na Wanasheria waliobobea Barani Afrika, ambao kwa mujibu wa rekodi zao zinaonyesha uadilifu na weledi kwenye maamuzi wanayoyatoa.