Ofisa Magereza Moshi apandishwa Kizimbani kwa kesi ya Ulawiti

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

5 hours ago
rickmedia: ofisa-magereza-moshi-apandishwa-kizimbani-kwa-kesi-ulawiti-172-rickmedia

Ofisa wa Magereza, Emmanuel Nyange (35) amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro akikabiliwa na kesi ya kumlawiti mtoto wa miaka 13.

Ofisa huyo amefikishwa mahakamani hapo Juni 24, 2025 mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ruth Mkisi na kusomewa shitaka moja la ulawiti.

Juni 14, 2025 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Abel Mtagwa alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema taratibu za kijeshi dhidi ya askari huyo zinaendelea na zitakapokamilika hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.