Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Nadia Mukami ametangaza kupumzika shughuli za kimuziki kwa muda wa wiki kadhaa baada ya kuanguka kwenye jukwaa la #OktobaFest.
Nadia ambaye ni mama wa mtoto mmoja amebainisha hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, kwa kuweka wazi kuwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la pumu kwa muda mrefu na kitendo cha kuanguka jukwaani kimemfanya atafakari zaidi juu ya afya yake.
“Jana Wakati wa #OktobaFest nilikuwa na na vibes kwenye jukwaa hadi kifua changu kikashindwa kustahimili tena na nikapata shambulio la pumu na Kuanguka nilipokuwa nikirudi nyuma ya jukwaa! Nimekuwa mgonjwa kwa muda na baada ya wikendi hii nitapumzika hadi tarehe 15 ili kutunza afya yangu! Asante sana.,”amendika mrembo huyo.