Tetesi: Gachagua kuhamia Chama pinzani, ahamasisha Gen Z kupiga kura kwa wingi 2027

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: tetesi-gachagua-kuhamia-chama-pinzani-ahamasisha-gen-kupiga-kura-kwa-wingi-2027-255-rickmedia

Naibu Rais aliyeondolewa Madarakani, #RigathiGachagua amedaiwa kukutana kwa siri na Viongozi wa Upinzani akiwemo #KalonzoMusyoka ikielezwa wanajadili mipango ya Uchaguzi wa Mwaka 2027.

Mtandao wa The Star umeripoti kuwa Gachagua ameanza ushawishi kwa Vijana wa Gen Z kuhakikisha wanajiandikisha ili washiriki Uchaguzi huo akiamini wao ndio silaha ya eneo la ukanda wa Mlima Kenya ambalo linatajwa kumpa ushindi Rais Ruto katika Uchaguzi uliopita.

Taarifa zaidi zinadai Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinatarajia kumfuta uanachama Gachagua ambaye amekuwa akipinga Sera za Rais Ruto hadharani