Afisa Mtendaji Mkuu wa Telegram, #PavelDurov, ametoa ofa ya matibabu ya bure ya In Vitro Fertilisation (IVF) kwa wanawake wanaokubali kutumia mbegu zake, Ofa yake ni juhudi ya kusaidia wanawake wanaopambana na changamoto ya kutopata watoto.
Mbali na kutoa mbegu, #Durov pia atagharamia taratibu zote za IVF kupitia ushirikiano wake na clinic uzazi ya Altravita,Clinic hiyo imeahidi kutoa huduma ya kiwango cha juu, ikishirikiana na wataalamu bora katika afya ya uzazi na kutumia teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha matokeo bora.
Mchakato kwa wanawake wanaotaka kushiriki ni rahisi lakini una hatua za kuchagua. Watu wanaopendezwa wanaweza kuwasiliana na Altravita kupanga mashauriano ya awali.
In vitro fertilization (IVF) ni muunganiko wa yai la mwanamke na manii ya mwanaume bila kujamiiana