Imeelezwa kuwa Wananchi wamepiga Kura ya ‘Ndio’ kwenye Mabadiliko ya Katiba yaliyopendekezwa na Serikali iliyomuondoa madarakani Ali Bongo na kumteua Jenerali Brice Oligui Nguema kuongoza taifa hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Hermann Immongault, Mabadiliko hayo yamepitishwa kwa 91.8% na takriban 53.5% ya Wananchi waliojitokeza kushiriki Mchakato huo, ikiwemo kuweka Mihula ya Vipindi Viwili.
Hata hivyo, Katiba haijamzuia Rais wa mpito (Jenerali Nguema) kugombea tena, hali iliyoibua hisia kuwa anaweza kurejea Madarakani akitokea kwenye Serikali ya Mpito badala ya Serikali ya Kiraia.