Jonas Mkude Ashindwa Kesi Ya Kumdai Mo Dewj Bilioni 1

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 month ago
rickmedia: jonas-mkude-ashindwa-kesi-kumdai-dewj-bilioni-933-rickmedia

Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya madai ya fidia ya Sh1 bilioni iliyofunguliwa na kiungo wa Yanga, Jonas Mkude dhidi ya kampuni ya Mohamed Enterprises (Tanzania) Limited.

Hukumu ya kesi hiyo namba 192 ya mwaka 2023 ilitolewa Juzi, Jumatano, Oktoba 30, 2024 na Jaji Phillip Butamo aliyeisikiliza baada ya kuridhika kuwa mdai, Mkude, ambaye ni kiungo wa Yanga hakuweza kuthibitisha madai yake.

Katika kesi hiyo, Mkude alikuwa akiidai kampuni hiyo inayoongozwa na rais wa Heshima na mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji (Mo Dewji) fidia ya Sh1 bilioni kwa madai ya kutumia picha ya sura yake katika matangazo ya biashara zake bila ridhaa yake.

Katika hati yake ya madai pamoja na ushahidi wake, Mkude aliyewahi kutumikia Simba kabla ya kuhamia Yanga, alidai kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikitumia picha ya sura yake katika matangazo ya kibiashara ya huduma na bidhaa zake bila ridhaa yake.

Alidai kuwa kampuni ilikuwa ikitangaza matangazo hayo kupitia mitandao yake ya kijamii ya Instagram, Facebook na Twitter (sasa X) nchini na duniani kote.

Mkude alidai kuwa Julai 12, 2023, akiwa amejiunga na Yanga wakati akijiandaa na mechi ya soka iliyokuwa mbele yao alibaini kuwepo kwa matangazo ya kibiashara yenye picha ya sura yake katika mitandao ya Kampuni hiyo.

Alidai kuwa aliyapiga picha na kuyahifadhi kisha baadaye aliyachapisha kwa uchunguzi zaidi na kwamba siku hiyohiyo alianza kupokea

simu na ujumbe wa maneno kwa njia ya simu kutoka kwa watu mbalimbali wakipongeza kwa fursa hiyo.

Mkude alidai kuwa mkataba wake na Yanga ulikuwa unamzuia kujihusisha na taasisi au klabu nyingine yoyote bila kupata kwanza ridhaa ya Yanga na kwamba kama kuna timu ya soka ilitaka kufanya naye kazi ilipaswa kuilipa Yanga Dola 100,000 za Marekani Kutokana na hali hiyo alifungua kesi hiyo dhidi ya kampuni hiyo akidai kuwa kwa kitendo hicho ilikiuka haki zake mbalimbali ikiwemo haki ya faragha na kuingilia haki zake za kiuchumi isivyo halali na akaomba

malipo ya fidia ya kiasi hicho pamoja nafuu nyinginezo.

MELT katika utetezi wake pamoja na mambo mengine ilidai kuwa ina haki ya kutumia picha ya Sura ya Mkude akiwa amevaa Jezi a Klabu ya imba kutangaza Bidhaa zake chini ya Mkataba wa udhamini na masoko kati yake na kampuni dada yaani A-One Product and Bttles Limited na Simba.