Waziri Mkuu wa zamani wa Baghladesh (Khaleda Zia) afariki Dunia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: waziri-mkuu-zamani-baghladesh-khaleda-zia-afariki-dunia-239-rickmedia

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh na kiongozi wa chama cha Bangladesh Nationalist Party (BNP) Bi.Khaleda Zia, amefariki akiwa na umri wa miaka 80.

Habari hii imetolewa rasmi na chama chake na vyombo vya habari vya kimataifa leo, Desemba 30, 2025.

Khaleda Zia ndiye Waziri Mkuu wa Kwanza mwanamke nchini Baghladesh,Chama chake cha upinzani cha Bangladesh Nationalist Party (BNP) kilisema kwamba alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na ugonjwa wa cirrhosis ya ini, arthritis, kisukari, na matatizo ya kifua na moyo, madaktari wake walisema.