Msanii wa muziki wa Bongoflava kutoka Tanzania Mbosso Khan ametazama maoni tofauti tofauti ya wadau wa sanaa nchini Tanzania kuhusu uwezo wake kimuziki na ameamua kuwaachia swali ili wampe majibu, wanahisi uwezo wake umetokana na nini?
Mbosso kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha zake na kuwauliza mashabiki wanadhani uwezo wake kimuziki unatokana na nini, Je ni kipaji,Mganga wake mzuri , Anabahatisha , Kaiba Daftari La Ya Moto Band , Akili Mnemba (AI) , au Anaandikiwa ….? wamuandikie majibu kwenye uwanja wa maoni(Comments) ila wengi wamejibu kwa kuandika Mbosso Khan uwezo wake unatokana na kipaji alichobarikiwa na Mwenyezi Mungu.
Ikumbukwe Mbosso amekuwa akisifiwa sana kwa namna alivyo hodari wa kutunga mashairi matamu yenye ladha kwenye nyimbo zake na hata alizoshirikishwa, hivi karibuni amesifiwa sana baada ya kuweka ubeti (Verse) mzuri sana kwenye wimbo wa Harmonize (Leo).
Je kwa upande wako wewe unahisi uwezo wa msanii Mbosso Khan unatokana na nini hasa kati ya vitu hivyo kadhaa alivyoviorodhesha??