Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ametumia mamlaka yake kwa mujibu wa Ibara ya 45(1)(a–d) ya Katiba ya 1977 kutoa msamaha kwa wafungwa 1,036 katika maadhimisho ya Miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba 2025.
Kati ya hao, wafungwa 22 wameachiwa huru kabisa, huku 1,014 wakipunguziwa adhabu na kuendelea kutumikia vifungo vilivyosalia.