Jeshi la Polisi yatoa taarifa ya usalama nchi siku ya uhuru 9 Disemba

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 days ago
rickmedia: jeshi-polisi-yatoa-taarifa-usalama-nchi-siku-uhuru-disemba-396-rickmedia

Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini Kutoka kwa Msemaji wa Jeshi hilo David Misime kuhusu hali ya usalama nchini leo ikiwa ni siku ya Uhuru 9 Disemba ambayo baadhi ya watu wenye ushawishi mitandaoni walitangaza maandamano ya amani yasiyo na kikomo.

Msemaji wa jeshi la Polisi amewataka watanzania kupuuza video inayowaonyesha wamaasai wengi huku ikiambatanishwa na ujumbe kuwa wamaasai hao wameandamana,Kamanda David Misime amesema video hiyo ipuuzwe kwani haina ukweli wowote wamaasai hao walikuwa kwenye sherehe zao za jando katika msitu wa tanapa.

Kamanda Misile pia amewataka watanzania kupuuza video zingine zinazoonyesha watu wameandamana kwani ni video za matukio ya nyuma hasa Oktoba 29 na mlengo wake ni kuvuruga amani,lakini pia jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuendelea kufuata sheria kwa usalama wa raia wote.