Kiongozi wa Upinzani Cameroon akimbilia Gambia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: kiongozi-upinzani-cameroon-akimbilia-gambia-965-rickmedia

Kiongozi upinzani nchini Cameroon, Issa Tchiroma Bakary, amekimbilia nchini Gambia, kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Gambia iliyotolewa hapo jana.

Tchiroma, aliyegombea urais katika uchaguzi wa Oktoba na ambaye anapinga matokeo yaliyomrejesha madarakani Rais Paul Biya, anadaiwa kuwasili nchini Gambia tangu Novemba 7 kwa misingi ya kibinadamu na kwa lengo la kulinda usalama wake.

Hatua hiyo inakuja wakati majadiliano ya kidiplomasia na juhudi za kusaka suluhu ya amani kuhusu mvutano wa baada ya uchaguzi nchini Cameroon yakiendelea. Tchiroma anasisitiza kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi huo, na mara kadhaa aliwahamasisha wananchi kuandamana kupinga matokeo.

Wakati huohuo, Serikali ya Cameroon imesema itamfungulia mashtaka ya kuhamasisha maandamano, ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu na kusimamisha shughuli mbalimbali nchini humo.