Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nchini Zuchu ameandika historia mpya baada ya kufikisha jumla ya views bilioni 1 kwenye mtandao wa YouTube.
Zuchu anakuwa msanii wa kwanza wa kike nchini kuwahi kufikia idadi hiyo kubwa ya watazamaji, hatua inayoonyesha ukubwa wa ushawishi na umaarufu wake barani Afrika.
Rekodi hii mpya inaendelea kuthibitisha nafasi ya Zuchu kama miongoni mwa wasanii wakike wenye mafanikio makubwa zaidi katika muziki wa Bongo Fleva.