Mbunge Marjorie Taylor Greene ametangaza kujiuzulu nafasi yake katika Bunge la Marekani, akisema mazingira ya kisiasa yamekuwa magumu na yenye mgawanyiko mkubwa tangu kurejea kwa Rais Trump madarakani.
Greene, mshirika wa zamani wa Trump, amesema amechukua hatua hiyo baada ya kuitwa msaliti na Rais na kuona uwezekano wa kuingia kwenye mchujo mgumu ndani ya Republican.
Pia amekuwa akitoa wito wa kufunguliwa kwa nyaraka za Jeffrey Epstein, jambo lililozua mjadala mkali. Ataondoka rasmi bungeni Januari 5, 2026. Trump amesema kujiuzulu kwake ni habari njema kwa nchi.