Klabu ya Simba Sc imetangaza kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande zote na Meneja Mkuu Dimitar Pantev pamoja na wasaidizi wake wawili, kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya katika CAF Champions League.
Taarifa kwa umma iliyotolewa , 2 Disemba 2025, na Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo inasema uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili. huku watu wakiamini kuvunjwa huko kwa mkataba kumelenga kuboresha mwenendo wa timu baada ya kuporomoka kwa matokeo katika mechi za hivi karibuni barani Afrika. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kocha Selemani Matola ametangazwa kuchukua uongozi wa kikosi kwa muda, wakati mchakato wa kumsaka kocha mwingine ukiendelea.
Pia hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Simba kukumbana na kipigo katika mechi mbili mfululizo 1- 0 dhidi ya Petro de Luanda, kisha kupoteza tena kwa mabao 2-1 mbele ya Stade Malien.
Matokeo hayo yameiacha Simba katika presha kubwa kwenye msimamo wa kundi kwani hawana alama yoyote katika kundi lao mpaka sasa.