Mwamuzi, Ahmada Simba aliyechezesha mchezo kati ya Yanga dhidi ya Fountain Gate ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa mizunguko mitano, baada ya kubainika kushindwa kutafsiri kwa usahihi sheria za mpira wa miguu.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Desemba 8, 2025 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (KFU) ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) imeeleza kuwa kosa hilo lilitokana na mwamuzi huyo kutoa adhabu ya penalti kwa Fountain Gate katika tukio ambalo, kwa mujibu wa kamati, halikustahili adhabu hiyo.
“Kamati imeridhia kuwa mwamuzi hakutafsiri vyema sheria husika na amepisha uamuzi uliokuwa na athari moja kwa moja kwenye matokeo ya mchezo,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.