Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, ameagiza IGP Camillus Wambura kuhakikisha ukamataji wa watuhumiwa unafanywa kwa kufuata taratibu za kisheria.
Amezuiwa Polisi kufanya ukamataji kwa kutumia vifunika uso (ninja), bila sare na wakiwa na silaha kubwa. Amesema ukamataji ufanyike kwa staha, mchana, na kwa taarifa wazi bila kusababisha hofu kwa familia za wanaokamatwa.
Pia amekosoa tabia ya kukamata watu kwa makosa madogo kama post ndogo mitandaoni, akisisitiza kuwa vitendo hivyo vinachochea chuki dhidi ya Polisi, wakati Jeshi hilo ndilo linahakikisha usalama wa wananchi.