DAWASA yatangaza upungufu wa maji Dar-Es-Saalam,yaeleza hatua ilizochukua

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

14 hours ago
rickmedia: dawasa-yatangaza-upungufu-maji-dar-es-saalamyaeleza-hatua-ilizochukua-710-rickmedia

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa), imesema wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini kumekuwa na upungufu wa huduma ya maji katika maeneo mengi.

Imetaja maeneo yanayohusika kuwa ni kuanzia Bagamoyo, Tegeta, Boko, Mbezi Beach, Mwenge, Kinondoni, Mwananyamala, Masaki hadi Ilala.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Desemba 6, 2025 na Kitengo cha Mawasiliano cha Dawasa, kimesema hali hiyo inatokana na uzalishaji wa Maji kushuka zaidi ya kiwango cha kawaida huku sababu ya kushuka kina cha Mto Ruvu na kuchelewa kwa mvua vikitajwa.

Hata hivyo kuhusu mtambo wa Ruvu Juu katika maeneo ya kuanzia Kibaha, Kibamba, Kimara, Tabata, Kinyerezi, Pugu hadi Kisarawe, mamlaka hiyo imesema hali ya uzalishaji maji inaendelea vizuri na huduma inawafikia wananchi.

Kutokana na hilo imesema kuwa jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa kwa kushirikiana na Wizara ya Maji ikiwemo kusitisha matumizi ya Maji ya Mto Ruvu kwenye shughuli za Kilimo na kuyaelekeza katika matumizi ya Binadamu na kuongeza matumizi ya Visima ili kupunguza changamoto ya kihuduma.