Muimbaji kutoka Nigeria Ayra Starr amethibitisha kuwa rasmi haishi tena Nigeria, kwani tayari amehamia jijini New York, Nchini Marekani.
Amesema licha ya kuhamia New York kwa muda usiozidi miezi miwili, amekuwa akikaa huko mara nyingi kwa sababu jiji hilo linamkumbusha Lagos, na kuna Wa-Nigeria wengi hivyo huhisi kama yuko nyumbani tu.
Pia Ayra ameeleza kuwa mji huo unampa uhuru wa ubunifu, fursa nyingi za studio, na mazingira mazuri kwa ushirikiano wa kimataifa.