Muigizaji kutoka Japan Cary-Hiroyuki Tagawa, amefariki dunia akiwa na miaka 75 kutokana na matatizo ya kiharusi.
Taarifa kutoka kwa mwakilishi wake zinasema alifariki Alhamisi mjini Santa Barbara, akiwa ameungana na familia yake.
Alianza kujulikana zaidi kwa nafasi yake ya Shang Tsung katika filamu ya Mortal Kombat (1995) pia Tagawa alitamba Hollywood kwa zaidi ya miaka 40, akishiriki katika zaidi ya filamu 30, ikiwemo The Last Emperor (1987), License to Kill (1989), Rising Sun (1993) na Pearl Harbor (2001).
Pia alipata umaarufu kupitia nafasi ya Nobusuke Tagomi katika mfululizo wa The Man in the High Castle, Ameacha watoto watatu na wajukuu wawili.