Serikali ya Korea Kusini kutoa Milioni 93 kwa wananchi wake watakao funga ndoa na kupata watoto

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: serikali-korea-kusini-kutoa-milioni-kwa-wananchi-wake-watakao-funga-ndoa-kupata-855-rickmedia

Serikali ya Korea Kusini imetangaza motisha kubwa za kifedha ili kukabiliana na mdororo wa idadi ya watu, ikilenga kuhimiza mahusiano, ndoa na uzazi.

Baadhi ya serikali za mitaa zinatoa ruzuku za uchumba, bonasi za ndoa, msaada wa nyumba na malipo ya moja kwa moja kwa wazazi.

Hatua hizi zinalenga kupunguza gharama za maisha ambazo zinatajwa kuchelewesha au kuzuia ndoa na kupata watoto, wakati nchi ikikabiliwa na kiwango cha chini zaidi cha uzazi duniani.