Msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania Rajabu Kahari maarufu kama Harmonize ambaye amekuwa na mahusiano ya kuachana na kurudiana kwa muda mrefu na Mwigizaji Kajala Masanja inasemekana leo hii Disemba 29 anatarajia kumvisha pete tena mrembo huyo baada ya kurudiana tena Disemba 25 mwaka huu 2025.
Kwa mujibu wa post ya Mwijaku ambaye yupo karibu na familia ya Harmonize anasema jambo hilo linatarajiwa kufanyika leo hii huku akisisitiza wawili hao kuheshimu kiapo hicho kwani wakienda tofauti na hapo umauti unaweza kumkuta mmoja wao kwa mujibu wa ndoto yake.
Watu wanajiuliza je ni sahihi Harmonize kumvisha pete tena mrembo huyo kwani Harmonize na Kajala walivishana pete ya uchumba mwaka 2022 na kabla yakuifikia hatua ya ndoa wawili hao waliachana.
Kama kweli wanavishana pete leo hii basi Mungu awasaidie wafikie hatua ya ndoa moja kwa moja.