Beyoncé ameandika historia baada ya kuthibitishwa kuwa mwanamuziki wa tano duniani kufikia utajiri wa dola bilioni moja (USD 1B). Mafanikio haya yametokana na ziara zake kubwa, uwekezaji wa biashara, pamoja na mwelekeo wake mpya wa muziki wa country kupitia albamu yake Cowboy Carter iliyovunja rekodi na kupokelewa vyema kimataifa.
Baada ya taarifa hizo, baba yake Mathew Knowles alijitokeza hadharani na kuandika ujumbe mfupi lakini mzito kihisia, akionesha fahari yake kwa mafanikio ya binti yake. Mathew aliandika:
“Ninajivunia sana binti yangu, amefanya kazi kwa bidii na imezaa matunda.
Beyoncé sasa ni bilionea.
Uamuzi wake wa kishujaa wa kugeukia muziki wa country umezaa matunda makubwa, ukiongoza hadi kwenye ziara yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya muziki wa country, na kusaidia mradi wa Cowboy Carter kumuingizia mapato ya kiwango cha juu (dola za tarakimu 10).
Mafanikio hayo yamemfanya Beyoncé kuwa mwanamuziki wa tano tu duniani kufanikisha jambo hilo.”x

Ujumbe huo umeamsha hisia kwa mashabiki wengi, wakitaja safari ya Beyoncé kama mfano wa nidhamu, uvumilivu na maamuzi sahihi ya muda mrefu. Kwa sasa, Beyoncé anaungana na majina makubwa kama Jay-Z, Rihanna, Taylor Swift na Paul McCartney kwenye klabu adimu ya wasanii waliothibitishwa kufikia hadhi ya ubilionea.