Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuvuliwa silaha kwa Hamas ni sharti kuu la kuanza awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa amani ya kudumu na ujenzi mpya wa eneo hilo.
Kauli hiyo imetolewa baada ya mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, huku Trump akisema Israel imetekeleza majukumu yake ya awamu ya kwanza na sasa shinikizo likiwa kwa Hamas.
Marekani imeahidi kuendelea kushinikiza utekelezaji wa sharti hilo licha ya wasiwasi wa kuvunjika kwa makubaliano.