Watumiaji wa 'ICloud ' Uingereza wafungua madai ya Tsh.Tril 10 dhidi ya Apple

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

6 days ago
rickmedia: watumiaji-icloud-uingereza-wafungua-madai-tshtril-dhidi-apple-859-rickmedia

Kampuni ya Apple inayozalisha Vifaa vya Kidigitali zikiwemo Simu za #iPhone, iPads na Laptop, imefunguliwa Kesi ya Madai ya takriban Tsh. Trilioni 10.19 ikidaiwa kulazimisha Wateja kutumia huduma za iCloud.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Kundi la Watumiaji Huduma liitwalo ‘Which?’ inaituhumu Apple kukiuka Sheria ya Ushindani kwa kuwataka Wateja kuhifadhi Data zao kama Picha au Video kwenye #iCloud na kulipia gharama wanapohitaji kuongeza nafasi ya uhifadhi au kupata data zao.

Apple imekuwa ikitoa Hifadhi ya Mtandaoni (Cloud Storage Space) yenye ukubwa wa Gigabytes 5 (5GB) kwa wateja wa Vifaa vyake, lakini imeweka sharti la malipo ya takriban Tsh. 40,416 kwa nyongeza ya Gigabaiti 50 na Tsh. 2,245,308 kwa Terabaiti 12 kwa mwaka.