Kiongozi wa Upinzani na Mkosoaji mkubwa wa Rais Museveni, Dkt Kizza Besigye pamoja na mshirika wake, Hajj Obeid Lutale wameshtakiwa katika Mahakama ya Kijeshi Jijini Kampala kwa kumiliki silaha Nchini Kenya, Ugiriki na Uswisi
Wawili hao walikamatwa kwa nguvu wakiwa Nchini Kenya mwishoni mwa Wiki iliyopita, ambapo taarifa za kukamatwa kwao zilitolewa na Mke wa Kizza, Winnie Byanyima kupitia Mitandao ya Kijamii, akisema Mumewe alitekwa nyara Siku ya Jumamosi huko Nairobi.
Wakili wa Dkt. Kizza, Eria Lukwago ameliambia Shirika la Habari la AFP kwamba kesi ya Besigye (68) imeahirishwa hadi Desemba 2, 2024, baada ya Mwanasiasa huyo kupinga kesi hiyo, akisema raia wa kawaida hatakiwi kushtakiwa kwenye Mahakama ya Kijeshi, pamoja na kukosa uwakilishi wa Mawakili kutokana na kuzuia kufanya Mawasiliano na Mtu yeyote.