Kongamano la Maaskofu wa Katoliki Kenya (KCCB) limepinga vikali pendekezo la kuongeza muda wa Urais kutoka Miaka Mitano hadi Saba wakidai ni pendekezo lenye ubinafsi kutokana na tamaa ya viongozi wa kisiasa nchini humo.
Pia, Maaskofu hao wamekosoa Sera za Kodi za Serikali wakidai zinatozwa kupita kiasi na kuathiri uchumi wa Wananchi kufuatia maandamano ya kupinga Bajeti ya Muswada wa Fedha, Juni 2024.
Aidha, wameungana na vikundi vya Binadamu kulaani vitendo vya utekaji wakidai ni ukiukwaji wa Haki za Binadamu na uminyaji wa uhuru wa kujielezea na hivyo wanahimiza Serikali kuchukua hatua haraka kulinda usalama na uhuru wa raia wote wa Kenya.