Jeshi la Polisi limesema linachunguza Video iliyosambaa Mitandaoni ikionesha Watu wanaotaka
Kumkamata na Kumwingiza kwenye Gari Mfanyabiashara #DeogratiusTarimo ambaye amesharipoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Gogoni Imeelezwa kuwa Manyabiashara huyo alifika katika Hotel ya Rovenpick, Kiluvya kufanya mazungumzo ya
Kibiashara na Watu hao ambao alikuwa akiwasiliana nao tangu Oktoba 25, 2024.
Polisi imesema itahakikisha inawakamata waliojaribu kufanya tukio hilo kulingana na ushahidi ambao umeshakusanywa na unaoendelea kukusanya ili hatua za Kisheria zichukuliwe.
Polisi yaanza Uchunguzi wa picha mjongeo inayoonesha Watu wakijaribu kumkamata na kujaribu kumwingiza Kwa nguvu Ndani ya gari Bw. DEOGRATIUS TARIMO ambaye ni Mfanyabiashara na Mkazi wa Kibaha Pwani. pic.twitter.com/UaHJfYmYDS